Katika karne hii ya ishirini na moja, karne ambayo sayansi na techenolojia ndio chombo pekee mbadala. Karne ambayo internet inawasogeza walio mbali kuwa karibu, internet inawavutia wasio na sauti kuwa na sauti, karne ambayo internet inawapa habari wasio na habari.
Hali ni tofauti nchini Tanzania, baadhi ya Wanatanzania wenzetu walishikiliwa na usalama wa Taifa kwa kisa cha kutumia haki yao ya kuongea pasipo kuvunja sheria.
Serekeli ya Mh. Jakaya Kikwete imetumia udictator kukamata raia wasio na hatia kwa kisingizio cha usalama. Mambo haya ya kinazi tumeyaona kwenye enzi za Hitler, na enzi za umoja wa nchi za Urusi katika karne hizo. Ni wazi kwamba CCM wanashindana na watu wasio wafahamu, ni sawa na kupigana na upepo. Kukamata wachangiaji katika internet sio dawa ya kuzuia watu kuzungumza mawazo yao, bali ni chachu ya kuwaamsha watanzania wengi kuingia kwenye mchakato huu.
Ni imani yangu kwamba serikali ya Mh. Jakaya Kikwete itawapa immunity hawa Watanzania wenzetu, na kukomesha mchezo huu wa kinazi kwa Watanzania wengine. Ni fika ya kwamba katika dunia ya leo Tanzania haiwezi kuafford adhabu za kuzuia haki ya uhuru wa kuzungumza.
Tanzania haiundwi na kundi la watu kumi au elfu moja, Tanzania inaundwa na watanzania zaidi ya million 36, hivyo kila mtanzania ana haki ya kuzungumza lile adhanialo ni muhimu kwa maoni yake pasipo kuvunja sheria. Watanzania hawa hawajavunja sheria, hivyo basi tunaomba waachiwe mara mmoja na wafutiwe mashitaka dubya yaliyoanzishwa.
Ni wazi kwamba Mh. Jakaya Kikwete amesifika katika Dunia kwa kuipa media haki ya uhuru, japokuwa swala hili limetia doa kwa serikali ya Mh. Jakaya Kikwete. Vilevile ni ufahamu wangu kwamba serikali ya Tanzania inafahamu nguvu ya internet, hivyo basi mimi kama Mtanzania natoa wito mmoja tuu, nao ni "Hao waliofunguliwa mashitaka wafutiwe mara moja" kabla hatujaomba msaada wa Internationa Media kama Associate Press kutusaidia kupressurize swala hili katika International Arena.
Lengo sio kuigawa Tanzania, Lengo ni kuunda Tanzania ya umoja na Amani. Tanzania inayoheshimu haki kwa wote, Tanzania inayofuata kanuni na misingi za uhuru wa wananchi. Karne hii ya ishirini na mmoja tunaitaji kwenda mbele na sio kurudi enzi za communism.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Mkuu hongera kwa kututupa hewani ijapo kwa muda
ni kwamba ktk karne hii ubabe wa enzi za kikomunist umepitwa na wakati, ikichukuliwa kuwa jicho likishafunguka halina siri yaani wananchi tumeamka na uongo wa serikali (ccm) tumeutambua na ghiliba zao zooote.
Je nini kimefanyika mpaka sasa kuhusu wenzetu wawili walio under custody ya polisi??
soma hii nimeitoa KLH news
37. ujumbe umefika kwa marafiki wa JF wakubw
Written by mwanahabari, on 20-02-2008 15:33
Jamani I am sure JF itakuwa online soon, nimeongea na wazee wanaopenda sana kusoma hii na wanawaunga mkono kabisa, nikisikia wamegundua nini kinachoendelea nitaaambia, hasa kuhusu wanachama wle wawili.
Post a Comment